Mtu akipita kwa nyumba iliokuwa ya waziri amkuta Ali katika dirisha, anachungulia anamwamru mchunga kutandika frasi, ataka kwenda kutembea. Yule Mwarabu akamwita, Ali! Akamwitikia, na'am. Mbona u katika nyumba hii? Ali akamwambia, Sultani hakuniambia, uza ghali si uza rakhisi, ati? Nami nimekuza ghali.
Ahh! Yule Mwarabu akataajabu, gissi gani huyu Ali kuwa katika nyumba ya waziri mkubwa, lakini haithuru. Akakaa.
Akapita Mwarabu mgine akamkuta chini sebulani, akamwita, Ali! Akamwitikia, na'am. Akamwambia, mbona nakuona hapa, Ali? Akamwambia, hii si nyumba yangu? Gissi gani kuwa hii nyumba yako? Sultani ameniambia, uza ghali si uza rakhisi, nami nimekuza ghali ati.
Akaondoka yule Mwarabu, akaenenda hatta mwangoni kwa Sultani. Akamwambia, bwana wangu, seyedi yangu, nimekuta mtumwa wako, Ali, katika nyumba ya waziri wako, nikamwuliza—Ali! Akaitika, na'am. Unafanyaje katika nyumba hii wewe? Ali akanijibu, Sultani ameniambia, uza ghali si uza rakhisi, nami nimekuza ghali.
Yule Sultani akataajabu, ndio mambo alionitenda waziri, nami naye twalipana wahadi wa kutosha kumwuliza Ali, kumbe yeye amekwenda kumwuliza Ali, na mali yake kufilisika? Bassi sasa mbona amekosa kuwili, amekosa mali yake, amekosa na usultani. Na weye upesi enenda kamwita Ali aje. Ee Walla, Bwana.
Akitoka mbio kwenenda akamkuta Ali, ataka kuingia mashuani kwenda kutembea. Akamwita, Ali! Akamwambia, na'am. Akamwambia, upesi, unakwitwa kwa