Page:Swahili tales.djvu/332

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
312
UZA GHALI.

nitakwenda leo kupata usultani, kwani nimeyajua kwa akili yangu. Akakaa waziri hatta saa ya tatu Sultani amebarizi. Akitoka nyumbani mwake waziri hana kitu illa kanzu yake moja ilio mwilini mwake. Akatoka na furaha roho yake.

Akaenda hatta akafika mbele ya mwango wa Sultani. Watu waliopo na asikari jamii waliopo wakastaajabu. Ah! Waziri mkubwa, ndiye mwenyi mambo yote ya Sultani, anakuja kwa kanzu moja, hatta viatu miguuni hana. Hatta watu wanamtaajabu pasiwe mtu mmoja aliojua alionalo katika roho yake. Wale watu wajinga wakanena, labuda anafiwa na mkewe. Ndiye akaja vile kwa Sultani.

Akaondoka waziri, akamwambia, Subalkheiri Seyedina. Sultani akamwambia, Allah bilkheir al wazir, karib. Akakaa kitako.

Sultani akanena, nambie khabari zako, walizonazo. Akamwambia, khabari kheri, nimekuja kukupa maana ya maneno yako yale twalioahadiana mimi nawe, Sultani. Nami nimeyajua kwa akili zangu, Sultani.

Sultani akamwambia, nieleze la kwanza.

Akamwambia, yule Ali walipo watu waka'muliza, kwani mali yake yakafilisika, kuwaambia, asiojua maana haambiwi maana, kwa sababu wale watu wajinga hatawaambia maneno yale. Hawajui la kumjibu, bassi si afathali hawaambii wasiojua maana? Kwani mwenyi kumwambia mtu neno ataka kujibiwa. Utamwambia mtu neno hajui la kujibu? Bassi ndio maana yako asiwaambie. Sultani