Page:Swahili tales.djvu/330

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
310
UZA GHALI.

fungu moja nalitia baharini, funga moja nalipiga moto, fungu moja nalikopesha wala sitalipwa, fungu moja nimelipa deni wala sijaisha kulipa.

Bassi, nambie, Ali, maana ya kutosa baharini fungu moja, maana yake nini?

Ali akamwambia waziri, niwie rathi kwa killa nitakalonena stahamili. Akamwambia, baharini ni mali naliyokwenda kufanya usherati na waanaake, yamepotea mali yale sitayapata tena, bassi kama naliyotia baharini, kwani kitu kikizama bahari hakipatikani.

Na maana ya kupiga moto fungu moja?

Ali akanena, nalikula sana, nalivaa sana, nalitumia sana, ndiyo maana ya kupiga moto, kwani havitaregea tena katika mikono yangu.

Nambie fungu la tatu, maana ya kukopeshwa wala hutalipwa nini?

Akamwambia waziri, ni kama mtu waliompa mkeo mahari yake, haitarudi tena, bassi ndio maana ya kukwambia nimekopesha wala sitalipwa.

Akamwambia, fungu la nne nambie maana yake ya kunena umelipa deni wala hujaisha kulipa.

Akamwambia waziri, ni kama mtu aliompa mama yake mali kutaka kumfurahisha roho yake, walakini mimi mtoto sijui kama mama yangu nifurahi roho yake kwa haya naliyomtendea, bassi na mimi kijana hunena rohoni mwangu, hajaisha mama yangu kufurahi kwa yale naliompa mali. Ndio maana ya kukwambia, nimelipa wala sijaisha kulipa.

Akamwambia, ahsánt, Ali, na maneno yako nimeyasikia.

Nao kumekuwa jua lachomoza, saa kumi na mbili zimekwisha piga. Akakaa waziri na roho yako furaha,