Page:Swahili tales.djvu/312

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
292
MWALIMU GOSO.

mwambia, Wewe kupe mgandama ng'ombe, na ng'ombe mnwa maji, na maji mzima moto, na moto mla kisu, na kisu mkata kamba, na kamba mfunga paka, na paka mla panya, na panya mzua kiyambaza, na kiyambaza mzuia kusi, na kusi ikaangusha buyu, likampiga mwalimu wetu Goso, si mtende. Yule kupe akanena, kwamba mimi ni bora ningaliliwa ni paa?

Wakaenenda wakamtafuta paa, walipomwona wakamtwaa wakampiga. Yule paa akanena, mimi paa, mwanipiga, nimefanya nini? Wakamwambia, Wewe paa, mla kupe, na kupe mgandama ng'ombe, na ng'ombe mnwa maji, na maji mzima moto, na moto mla kisu, na kisu mkata kamba, na kamba mfunga paka, na paka mla panya, na panya mzua kiyambaza, na kiyambaza mzuia kusi, na kusi ikaangusha buyu, likampiga mwalimu wetu Goso, si mtende.

Yule paa asinene neno, akanyamaza. Wakanena, Huyu ndiye aliyeangusha buyu likampiga mwalimu wetu Goso, naswi na tuta'mua. Wakamtwaa yule paa, nao waka'mua.