Page:Swahili tales.djvu/310

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
290
MWALIMU GOSO.

mwalimu wetu Goso, si mtende. Kile kisu kikanena, kwamba mimi ni bora, ningaliliwa ni moto?

Wakaenenda wakautwaa moto, wakaupiga. Ule moto ukanena, mimi mwanipiga, nimefanya nini? Wakamwambia, Wewe moto mla kisu, na kisu mkata kamba, na kamba mfunga paka, na paka mla panya, na panya mzua kiyambaza, na kiyambaza mzuia kusi, na kusi ikaangusha buyu, likampiga mwalimu wetu Goso, si mtende. Ule moto ukanena, kwamba mimi ni bora, ningalizimwa na maji?

Wakaenenda wakayatwaa maji, wakayapiga. Yale maji yakanena, mimi mwanipiga, nimefanya nini? Wakamwambia, Wewe maji mzima moto, na moto mla kisu, na kisu mkata kamba, na kamba mfunga paka, na paka mla panya, na panya mzua kiyambaza, na kiyambaza mzuia kusi, na kusi ikaangusha buyu, likampiga mwalimu wetu Goso, si mtende. Yale maji yakanena, mimi kwamba ni bora, ningalinwiwa ni ng'ombe?

Wakaenenda, wakamtwaa ng'ombe, wakampiga. Yule ng'ombe akanena, Mimi mwanipiga, nimefanya nini? Wakamwambia, Wewe ng'ombe, mnwa maji, na maji mzima moto, na moto mla kisu, na kisu mkata kamba, na kamba mfumga paka, na paka mla panya, na panya mzua kiyambaza, na kiyambaza mzuia kusi, na kusi ikaangusha buyu, likampiga mwalimu wetu Goso, si mtende. Yule ng'ombe akanena, kwamba mimi ng'ombe ni bora, ningaligandamwa ni kupe?

Wakaenenda wakamtwaa kupe, wakampiga. Yule kupe akanena, Mimi mwanipiga, nimefanya nini? Waka-