Page:Swahili tales.djvu/306

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.

MWALIMU GOSO.


Palikuwa na mwalimu akisomesha watoto, tini ya 'mbuyu, jina lake huyu mwalimu yuwaita Goso. Hatta siku moja akaja paa, akakwea juu ya ule 'mbuyu, akaangusha buyu, likampiga yule mwalimu, akafa. Wale waanafunzi wakamtwaa mwalimu wao, wakaenenda, wakamzika.

Walipokwisha mzika, wakanena, Na twenende, tukamtafuta huyu aliyeangusha buyu, likampiga mwalimu wetu Goso, nasi tukimpata, tu'mue.

Kisha wakanena, Aliyeangusha buyu ni kusi, ilivuma ikaangusha buyu, likampiga mwalimu wetu, na twenende tukaitafute kusi, tuipige.

Wakaitwaa kusi wakaipiga. Ile kusi ikanena, mimi kusi, mwanipiga, nimefanya nini? Wakamwambia, Wewe kusi ndiwe uliyeangusha buyu, likampiga mwalimu wetu Goso, si mtende. Ile kusi ikanena, kwamba mimi ni bora, ningalizuiwa ni kiyambaza?

Wakaenenda wakatwaa kiyambaza, wakakipiga. Kile kiyambaza kikanena, mimi mwanipiga, nimefanya nini? Wakamwambia, Wewe kiyambaza mzuia kusi, na kusi