Page:Swahili tales.djvu/290

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
270
SULTANI MAJINUNI.

ndikia mauti yangu kuwa huku hatika mwitu. Akamwambia, mwanangu, lile nalilokwambia nifuate. Akamwambia, Ee walla, bwana wangu, mambo yote nitakufuata, bwana wangu, lakini hili moja nami nipe hisa. Akamwambia, enenda, lakini safari hii ukirudi hutakwenda tena. Akamwambia, nami, baba, nikiwa mzima hatta nikirudi, roho yangu imenihubiri siendi tena. Akamwambia vema, mwanangu.

Akaenda zake msitu na nyika, hatta akapita mwitu mkubwa, akiona kilima kikuu sana, na kule juu ya kilima, kuna kilele kikuu sana. Akaona njia inakwenda hatta imeshuka chini ya kilima. Akawaambia, Je! watumwa wangu, shauri yenu. Wakamwambia, kama ipi, bwana? Akawaambia, shauri ya kwanza, sasa hapa tuliopo sisi, nataka tupande mlima mkuu hatta tufike juu ya kilele, tutazame gissi yake mji, tuna nafasi kupata kwenda mbele. Wakamwambia, Bwana, mbona sisi hatuwezi kupanda katika mlima. Akawaambia, kama nyie mwaogopa, jua limekuchwa, na tulale hapa hatta kesho. Wakamwambia, vema, bwana.

Wakatwaa mabumunda pale, wakatwaa na mkate wa kusonga, wakala, wakatwaa na ladu, wakala, wakashiba, wakanywa maji, wakalala; wakapata usingizi mwema sana. Killa mtu hakufahamu hatta ussubui jua linachomoa, wakaamshana, haya, ondokeni kumekucha. Tufanye shauri kungali na mapema bado.

Wakamwambia, haya, bwana, tumeamka, tupe shauri yako. Akawaambia, shauri ya kwanza, na pike wali, tule. Akawaambia, twaa, mpekeche moto mpike wali, tule upesi. Wakapika wali pale, wakaisha, wakamwambia, Bwana, wali umekwisha. Akawaambia, kama umekwisha, pakueni.