Page:Swahili tales.djvu/286

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
266
SULTANI MAJINUNI.

Akawaambia, akina baba! Akawaambia, siku ya leo labuda ndio riziki yetu ya mwisho, bassi leo watu hutakana buriani, atakaopona atapona, na atakaokufa atakufa, lakini atakaopona kama mimi nimekufa, na akamwambie mama na baba asifanye msiba. Wakamwambia, haya bwana twende zetu tutapona inshallah.

Wakaenda zao kwa magoti, hatta wakifika pale kichakani, alipo. Wakamwambia, tupe shauri, bwana. Akawaambia, hapana shauri illa na tumpige tu marra moja. Wakampiga marra moja. Ndovu akawafukuza, killa akatupa bunduki yake aliokuwa nayo, hatta nguo waliovaa wakaziona nzito, wakazitupa kwa sababu ya kwenda mbio, killa mtu akapata mti akapanda. Ndovu akaenda zake akaanguka upande mwingine.

Wale wakakaa juu ya mti killa mtu tokea saa ya tissia hatta saa ya thenashara ussubui, hawana kula, hawana nguo, wamekaa kama siku walipozaliwa katika matumbo ya mama yao.

Yule kijana juu ya mti akalia sana. Akanena, mimi kama sijui kufa, ni huku leo kufa. Na killa mtu hamwoni mwenziwe. Yule kijana ataka kushuka juu ya mti aogopa, asema, labuda nunda yuko chini atanila, na wale watumwa wake vilevile, waogopa kushuka, wasema labuda nunda yuko chini atatula. Nao katika mwitu ulio mkuu, si pahali peupe.

Yule Kiroboto amemwona yule nyama alipoanguka, lakini aogopa kushuka peke yake, hunena, labuda pale alipoanguka, anena, yule mzima bado hajafa; hatta alipomwona mbwa anakuja kumnuka, akajua kama kweli amekufa.