Page:Swahili tales.djvu/282

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
262
SULTANI MAJINUNI.

amelala katika mti mkuu, akawaambia watumwa wake, leo tumemwona nunda yule. Yu wapi, bwana? Yule chini ya mti. Ee, tufanyeje, bwana? Akawaambia, sasa na tule kabisa, tupate kwenda kumpiga, tumempata vema, akituua, bassi. Wakamwambia, haya, bwana, wakatoa mabumunda, wakala hatta wakashiba. Akawaambia, na killa mtu na ashike bunduki mbili, moja iwe chini, moja iwe mkononi mwake. Wakamwambia, Ee walla, bwana. Akawaambia, na tupige marra moja hizi zote. Wakamwambia, Ee walla, bwana. Wakaenda polepole ndani ya miiba ile, hatta wakaingia katika mwitu pale, wakamtokea kwa mgongoni wakamjongelea hatta akawa karibu yao, wakampiga, risasi zika'mingia sana. Akatoka mbio yule faru pale alipopigwa, akaenda, akaangukia mbali kidogo. Wakamfuata, hatta wakamwona ameanguka amekufa. Wakamfunga, wakamkokota muda wa siku mbili njiani, hatta walipofika nuss ya njia wakaimba,

Mama wee, niulaga
Nunda mla watu. (Marra kumi.)

Mwanangu, si yeye
Nunda mla watu. (Marra saba.)

Wakaja watu wengi kumtazama yule faru, wakamsikitikia sana yule kijana.

Babaye na mamaye wakalia sana. Wakamwambia, baba ukae kitako. Akawaambia, baba yangu, naliokwambia halirudi nyuma, kama kufa mimi hivyo ninavyokwenda killa siku, nami nimekwisha kufa, lakini sijui, bassi niacheni, mimi.

Babaye akamwambia, ntakupa mali uyatakayo, ntakupa na enzi yangu, uwe wewe Sultani, mimi nishuke, nikae