Page:Swahili tales.djvu/272

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
252
SULTANI MAJINUNI.

usiku huja mjini, akakamata akipatacho na ufajiri akaenda shamba. Na killa watu wakimwendea kumpa khabari Sultani, kwa maneno ya paka, hawampati.

Akazidi kujongea mbele shamba yule paka, hukamata akipatacho, akipata kuku, akipata mbwa, akipata mbuzi, akipata ng'ombe, akipata mtu, cho chote kimpitiacho mbele yake hukamata, na asipokiona kitu cha kukamata hufanya juhudi ukitafuta, na usiku wa mjini, na ufajiri akaenda shamba. Kazi ikawa ileile, ya kukamata paka na Sultani hapatikani.

Hatta siku hiyo Sultani akanena, mimi leo natazama shamba, tendeni tukatazama, watoto. Akafuatana Sultani na watoto wale sita. Wakaenda hatta katika njia pana magugu, wale watoto sita huko nyuma, baba yao yu mbele. Yule paka akatoka katika mwitu, akiwaua watoto watatu. Watu wakaruka, paka! paka! paka! paka! Wakamwambia asikari, Je! Bwana tumtafute tu'mue. Akawaambia, tafuteni m'mue. Wakamwambia, Ee walla, bwana.

Akawaambia, huyu hakuwa paka tena, huyu jina lake nunda, aliokuja kunikamatia hatta waanangu. Wakamwambia, Bwana yule paka hatachagua, huyu mwana wa bwana, nimwache, ao huyu mke wa bwana nimwache, ao huyu jamaa yake bwana, nimwache; neno hili hakuna kwake la paka huyu kuchagua. Twakuchelea bwana hatta wewe kukula. Akawaambia, kweli hatta mimi atanila. Hatukwambia bwana, kama paka huyu anakwisha watu, ukanena, paka wangu na watu wangu? Akawaambia, kweli nimenena.

Wale asikari walipokwenda kumpiga yule paka, wangine