Page:Swahili tales.djvu/264

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
244
SULTANI MAJINUNI.

sha tende. Aliposikia maneno yale, yule mwanamke aliacha kupika akaenda mbio darini. Akamwambia, nini, bwana? Akamwambia, tazama katika dirisha. Alipotazama amwona mwanawe anakuja kwa furaha na wale watumwa, waliokuja kwa furaha.

Babake akaamuru asikari, mfuateni, mkamtwae mtoto. Wakaenda asikari mbio, wakaenda wakamchukua hatta akifika kwa babaye.

Je! khabari mwanangu. Akamwambia, sina khabari, khabari yangu ni kufunua kinwa hakulimbusha tende. Akamwambia, na'am, ndio kuzaa huku nilimbushe mwanangu. Akichuma tende, akamtia baba yake kinwani. Akachuma tende, akamtia mama yake kinwani.

Akamwambia, huku mwanangu ndio kuzaa, si kama wale wapumbavu, si kama wale asherati. Akamwambia, Je! mwanangu walimfanyaje ndege huyu, mwalimngojea wewe na nani, ndege huyu. Akamwambia, ndege huyu nalimngojea mimi peke yangu, nami hamwona tena, wala hatakuja tena maisha yake, na maisha yako, na maisha ya wangine watakaokuja.

Akamwambia, mwanangu, hapana jambo lalionipendeza kwako, kama hili walionilimbusha tende, kwani nimekaa miaka mitano mimi sikupata kulimbuka tende. Nami nna watoto sita, wala si mmoja, wewe naliokwambia mpumbavu ndio walionilimbusha tende. Hawa mimi siwataki.

Akaondoka mamaye akaenda kwa mumewe, akamwambia, si wakatae, mwenyi kukataa mwana hukataa mwana wa haramu, na wewe Sultani Majnuni, ukiwakataa watoto hawa, watu watawaambia waana wa haramu, na mimi