Page:Swahili tales.djvu/26

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
6
KISA CHA PUNDA WA DOBI.

mtoka, akanena, nyama imenona hii. Akaenda akamwambia simba. Na simba atoka ugonjwani, amekonda sana. Sungura akamwambia, ntakuleta nyama kesho, tuje tule. Akamwambia, vema.

Sungura akaondoka, akaenda mwituni, akamwona punda, na yule punda mke. Akamwambia, nimetumwa kuja kukuposa. Na nani? akamwuliza. Akamwambia, na simba. Akakubali, akafurahi sana punda. Akamwambia, Twende zetu, bass.

Wakaenda zao, hatta wakafika kwa simba. Akawakaribisha simba. Wakakaa kitako. Sungura akamkonyeza simba, akamwambia, nyama yako hiyo imekwisha kuja, nami naondoka. Akamwambia punda, nnakwenda chooni mimi, zumgumzeni hapo na mumeo.

Simba akamrukia, wakapigana, akapigwa sana simba kwa mateke, naye akampiga makucha mengi. Akaangusha simba akakimbia punda, akaenda zake mwituni. Akaja sungura, akamwambia, Je! simba, umempata? Akamwambia, sikumpata, amenipiga kwa mateke amekwenda zake, na mimi nimemtia madonda mengi, sababu sina nguvu. Sungura akamwambia simba, tulia we.

Wakakaa siku nyingi, hatta punda akapona madonda yale, na simba akapata nguvu sana. Akaenda sungura kwa simba, akamwambia, waonaje sasa, nikuletee nyama yako? Akamwambia, kaniletea ntaikata vipande viwili.

Akaenda sungura mwituni. Punda akamkaribisha sungura, akamwuliza khabari. Akamwambia, na mchumba wako anakwita. Punda akamwambia, siku ile umenipeleka, amenipiga sana kwa makucha, naogopa sasa.