Page:Swahili tales.djvu/258

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
238
SULTANI MAJINUNI.

Akamwambia, kunakucha, nataka kwenda zangu uniachie, mtoto, tafáthal nitakwenda zangu. Akamwambia, sikuachi kabisa leo, utakapopita ntapita nawe, utakapokaa ntakaa nawe, utakapokufa ntakufa nawe, lakini leo mimi sikwachi.

Akashuka ndege hatta chini, akamwambia, sasa umefika kwenu hapa, nami nipe ruhusa nende zangu. Akamwambia, sikwachi. Akamwambia, tafáthal mtoto uniache. Akamwambia, Ndugu zangu aliopewa ukaya, amepewa, aliopewa kisuto, amepewa, aliovikwa kanzu na barakoa, amevikwa, na yote haya hayangewapata illa kwa sababu yako wewe, kwa kuja kula tende.

Akamwambia, tafáthal, bassi kunakucha sasa bwana, nache, hichi kikomo cha leo, sitakuja tena hapa, wala sitakula tena tende hizi, wala sitapita tena mtaa huu, tafáthali kijana niache nende zangu.

Akamwambia, kama wewe hutaki kuniacha na tupane wahadi mimi nawe. Amwuliza, upi? Akamwambia, mimi nitakupa wahadi, niponye la jua, nikuponye la mvua. Akamwambia, mbona? Sikuamimi. Akamwambia, twaa haya maneno yangu, utakapopita po pote utanipata. Eh! ntakupataje? Akamwambia, ukitwaa hili nyoya, ukitia motoni nikisikia harufi yake, nitakapokuwa pahali gani nitakuja. Akamwambia, bassi nami kunakucha, tafáthali watu wasinione, niache niende zangu. Akamwambia, bassi kua heri, enenda zako. Akamwambia, rafiki yangu, kua heri sana. Amwambia, utakaponiita,