Page:Swahili tales.djvu/256

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
236
SULTANI MAJINUNI.

akaruka naye kijana, hatta akafikilia naye juu. Akamwambia yule ndege, Ee, binadamu, umenifuata hatta huku nalikofika, ukianguka hapa hatta utakapofika chini, umekufa zamani, bassi uniache nikaende zangu, nawe nikakwache kwenda zako. Yule kijana akamwambia, mimi leo hapa sikwachi, utakapokwenda pote nitakwenda nawe. Akamwambia, mimi tende zako sikula, nami niache nende zangu. Akamwambia, mimi leo sikwachi, mimi hapa leo ni kama kupe na mkia wa ng'ombe. Akamwambia, niache nende zangu kumekucha tena. Akamwambia, mimi leo naliokwambia husikii? mimi hapa sikwachi, labuda uniue. Akamwambia, ndugu yangu sita hawapendezi kwa baba kwa sababu yako wewe, huja akila tende, bassi ntakuachiani leo? Mimi leo baba yangu atakuona, na ndugu zangu sita watakuona, na mama yangu atakuona, na wote watu waliomo katika mji wetu watakuona, mkubwa kwa mdogo, mtumwa kwa mngwana, mke kwa mume, hawa wote watakuona leo, ndio roho ya baba yangu leo itafurahi.

Akamwambia nache, kunakucha, nami tende zako leo sikula, bassi utafathali ukanacha, nami nikaenda zangu, nawe ukaenda zako. Akamwambia, mimi hapa leo siachi, labuda uniue. Akamwambia, bassi wewe hutaki kunacha, nitakurusha nikupeleke mbali sasa.

Akaruka naye sana juu, hatta yule mtoto akiona chini kama nyota. Akamwambia, je! umekuona kwenu? Akamwambia, nakuona kama nyota. Nikikutupa hapa, wewe utasalia? Akamwambia, nastahiba uniachie nife, kama kukuacha leo, sikuachi kabisa, utaporuka hatta ukafika mbingu, nami leo sikwachi.