Page:Swahili tales.djvu/244

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
224
SULTANI MAJINUNI.

huyu mwenzangu; na mkifanya mzaha mtatiana vidole vya macho, kwa sababu kiza kikuu. Wakakimbia wale wote watumwa, wakaenenda wakaingia katika vibanda vyao, na wale vijana wakaondoka, wakaenda wakalala. Ndege akashuka akila tende akaruka akaenda zake.

Nao hawajaamka, na mvua haijaanuka, na tufani haijaondoka, wakalala wale hatta saa thenashara zikapiga, nao hawana khabari kama kumekucha, na mvua ingalikinya, na giza vilevile, na tufani vilevile imekaza. Wakalala, hatta saa moja ikapiga. Hatta saa ya pili akitolewa mtu mjini kwa baba yao—Chukua mwavuli huu enenda zako hatta shamba, gissi gani watoto hawa? Hatujapata khabari zao, wazima ao hawawezi, tutapata tende, hapana tende, uulize khabari zao, njoo twambie.

Akitoka na mvua yake hatta shamba. Akaenda akifikia kwa nokoa, hawajaamka, amefunga mlango, amelala. Akapiga, hodi! hodi!! hodi!!! Nokoa akamjibu, nani wewe? Akamwambia, mimi Hweduni. Ah! akamwambia, kufanya nini usiku wote na mvua hizi? Akamwambia, ninyi watu wa shamba ati, wajinga ninyi mna saa zenu katika nyumba. Akamwambia, Eh! Hweduni, unatucheka tutapata wapi saa, sisi watu wa shamba? Akamwambia, unazo saa kaisha si moja, si mbili. Akamwambia, hatta kuijua hiyo saa, mimi sijui. Akamwambia; huna majogoo, ndio saa ya shamba ati. Ukisikia jogoo anawika, jue kumekucha, ao ufajiri, bassi si saa yenu hizo?