Page:Swahili tales.djvu/236

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
216
SULTANI MAJINUNI.

ya kwanza ikipiga utaiona tende kinwani kwako ukila. Bassi atakapokaa hatta saa kumi haioni tende kinwani kwake akila, ao licha saa ya kumi, hatta miezi mitano, haipati tende kinwani mwake akila.

Bassi utafanyaje bwana? Akamwambia, mimi kwa babangu siendi, nitatoroka. Akamwambia, Bwana, utatoroka nini, afathali wenende, kama kutoroka, utatoroka hatta lini? Akamwambia, nitatoroka hatta baba yangu roho yake hatta iwe rathi. Akamwambia, Bwana, si vema kutoroka mngwana, afathali uende.

Akaenda hatta kwa babaye. Akamkuta hajaamka, akamngoja hatta akaamka. Je! nipe khabari za katika bustani, mwanangu. Akamwambia, sina zayidi ya khabari, khabari nalionao moja, khabari yangu za tende, zimeliwa na ndege. Ndizo khabari nalizo nazo, sina zayidi ya khabari. Utakavyo unitende. Wewe kisu, mimi nyama.

Akamwambia, niondokelee mbele uso wangu, sipendi kukuona. Akaondoka, akaenda zake. Akanena, Ahhh! mimi sikuzaa waana ni marathi. Marathi kuondoa tumboni mwana asiofaa mtu ulimwenguni, atanifaa ahera. Bassi waana hawa waana gani wasioweza kumtia mtu mchanga wa macho, kama ni kuzaa huku sizai tena.

Bassi akakaa kitako hatta mwaka mwingine, ukazaa mtende, na kulla mwaka huzidi kuzaa. Akanena alio mwanamume nitamwona katika bustani, tena nitamwona mkono wake kinwani mwangu akinilisha tende, ndiye nitakapomjua huyu mwanangu. Akawaambia, naye atakayenilisha tende, kijana huyu ntamwoza mke mzuri,