Page:Swahili tales.djvu/234

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
214
SULTANI MAJINUNI.

Sultani, tende linaanza kuiva. Akamwambia, haya, mwanangu, enenda katika bustani, kesho mwanangu utanilisha tende. Akamwambia, baba kesho saa ya kwanza ikipiga tende utaona katika kinwa chako unakula. Akamwambia, naomba miye mwanangu kesho nile tende hizi. Akamwambia, bassi, utakula baba, nami, kua heri, naenda zangu.

Akaondoka, akaenda zake. Hatta akawasili katika bustani, akawaambia wale watu walioko, killa mtu na alale nyumbani mwake asitoke. Tutakuachaje, Bwana, peke yako? Akawaambia, haithuru, niacheni, nimetaka mwenyewe. Wale watumwa wakaenda, wakalala. Na yeye akala, akaisha akalala, akalala sana, akiamka imekuwa saa sita, akakaa kitako chini ya mtende akicheza karata, yeye pekeyake, hatta alipokoma karibu alfajiri, ukampiga upepo mwema, akafanya kulala, usingizi ukimtwaa. Marra ndege akija akila tende zote, asisaze hatta moja, na yule mwenyewe amelala chini ya mtende na karata zake mkononi.

Hatta kulipopambazuka, nokoa wake akija, akamwona bwana wake amelala akitupa macho juu, aona tende hamna. Akamwita, Bwana! Bwana! Akamwitika, naam. Akamwambia, umelala, bwana, na tende ndani ya mtende hamna hatta moja, kama husadiki tupa macho juu utazame.

Alipotupa macho juu yule mtoto, akaanguka. Yule mtwana akisangaa alipomwona bwana wake ameanguka. Akimshika, akimwuliza, bwana, una nini? Akamwambia, nimekufa. Gissi gani, bwana kufa kwako? Kuja kwangu mimi huku shamba, nimemwambia baba yangu kama saa