Page:Swahili tales.djvu/228

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
208
SULTANI MAJINUNI.

atakula hizi, nitakaa mimi, kama yule mpumbafu akaja kulala usingizi burre, sasa baba amekwisha mchukia yule. Bassi mimi leo nitakaa hapa, nimtazame huyo ndege anaokuja kula tende hizi, nimwone mimi leo. Akakaa kitako akasoma sana. Akasikia majogoi yanawika, akautazame mtende akaziona tende zipo, akanena, Oh! baba yangu kesho atakula tende, athani mimi kama yule mpumbafu. Ukafanya kupambauka kidogo, ukampata usingizi. Akasema, Ah! nitegemee kidogo hapa penyi shina la mtende, usingizi ukamtwaa, ukimtwaa usingizi ndege akashukia mtende akala hatta asisaze hatta moja, naye yupo chini ya mtende, akalala, na msahafu wake kwapani.

Hatta kulipopambazuka akija yule nokoa wake, akiutazama mtende, hapana tende. Alipotupa macho chini akamwona bwana wake amelala chini ya mtende. Akamwambia, Bwana! Bwana! Akamwitikia, naam! Akamwambia umelala na tende zote zimeliwa na ndege. Kweli? Akamwambia, tupe macho juu, utazame. Akitupa macho, akaona tende hamna. Akasangaa, akili zake zimepotea, mashikio yake yameziba, miguu yake ikatetemeka, ulimi ukiwa mzito, akatekewa.

Akaondoka mtumwa wake akamwambia, Je! Bwana, una nini? Akamwambia, mimi mgonjwa sana leo. Akamwambia, kufa ku karibu kuliko kupona.

Akamwambia, ugonjwa wako gani, bwana? Akamwambia, mimi siumwi na kitwa, wala siumwi na tumbo, wala siumwi na ubavu, wala siumwi na mgongo, wala siumwi na kiuno, wala siumwi na miguu, wala siumwi na mikono,