Page:Swahili tales.djvu/226

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
206
SULTANI MAJINUNI.

hamna tende hatta moja. Nikiondoka nikienda hatta mtendeni hatazama haona kweli, hamna tende hatta moja. Bassi, khabari ni hizo za katika bustani, nami sina la zayidi.

Akamwambia, nimekuuliza khabari za katika bustani, umeniambia khabari mbili, umeniambia khabari njema na mbaya, mbaya nimekwisha kuziona kama tende zangu zimeliwa na ndege, bassi nambie na hizo njema. Akamwambia na hizi njema si miye mwana nimerudi salama? Akamwambia, si mwanangu sikutaki. Akamwambia, kana mwana wewe wa kula na kulala tu, utakapokuwa mtu atakapokwambia, wee baba twaa huu mchanga unitie wa macho, hutakubali wee. Bassi mwana gani wee? Sikutaki, enda zako, baba.

Akawaambia, safari hii ukizaa mtende wangu nitampeleka mtoto mwingine, hwenda akaungojea, hwenda nikapata tende nikalimbuka.

Akakaa muda wa miezi mingi, mtende ukazaa sana usichokuwa na kifani, ukakaa hatta karibu na kuiva, nathani, imesalia siku moja kuiva. Akatwaa mtoto akampeleka. Akamwambia, mwanangu nakupeleka katika bustani, natamani tende hizi mwaka huu kuzilimbuka. Akamwambia, baba yangu, nnakwenda zangu mimi sasa, hatta ussubui likikoma jua saa ya kwanza, mlete mtu aje akutwalie tende. Akamwambia, vema, mwanangu, napenda nilimbuke tende kesho.

Akaondoka mtoto akaenda zake. Hatta akafika bustani akalala sana hatta imekuwa tena, nathani, saa saba ya usiku, akiondoka akaenda hatta mtendeni, akaziona tende nzuri, matawi yananying'inia. Akauona mtende umesitawi sana, akanena. Ah! tende hizi babangu kesho