Page:Swahili tales.djvu/224

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
204
SULTANI MAJINUNI.

yamekuwa ya uwongo. Ah! nifanye shauri gani? Mimi nitakwenda zangu kwa baba nimwambie, walikuja Mabedui wakanifukuza, huku nyuma naliporudi tende nikitazama ndani ya mtende hamna. Ataniambia, watumwa wako wote wale msiwapige? Manenoye yamekuwa ya uwongo. Hatakubali mzee maneno haya. Mimi kesho nitakwenda kwa baba, nitamwambia, mtende mimi naliungojea hatta walipokuwa alfajiri, nako tena kunapambazuka haondoka enda kujinyosha kidogo, hatta nikipita mda kidogo kumekucha, nikimwona mtwana, akinijia akiniamsha, akaniambia, bwana, mtende hamna tende hatta moja. Nikiondoka, nikaenda hatta nikafika penyi mtende hautazama mtende, kweli, hamna tende. Bassi nami nimekuja kwako baba. Wewe kisu, mimi nyama, utakavyo vyote nitende. Haya ndiyo maneno mema, afathali kunena kweli, kama kunena uwongo.

Akaondoka hatta kwa babaye. Akamkuta babaye amekaa kitako barazini na watoto wake wale watano. Akija pale akimwamkia baba yake. Akamwambia, nipe khabari za katika bustani. Akamwambia, khabari njema mbaya. Gissi gani kuwa mbaya, gissi gani kuwa njema? Akamwambia, mbaya, ule mtende, tende zimeliwa na ndege zote, haikusaa hatta moja. Akamwambia, walikuwa wapi hatta mtende wangu ukaliwa na ndege? Akamwambia, mimi naliungojea mtende hatta alfajiri, na majogoi wanawika, tena kumepambazuka, haondoka pale kwenda kujinyosha kidogo, marra akinitokea nokoa, akaniamsha. Nikaamka hamwuliza, wataka nini? Akaniambia, wewe umekuja kuungojea mtende? Nikamwambia, nimekuja kuungojea mtende. Akaniambia bassi katika mtende