Page:Swahili tales.djvu/204

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
184
MOHAMMADI MTEPETEVU.

jabali, na chini yake mto unapita. Bassi tukashuka pale juu ya jabali. Niliposhuka nikamtafuta, nisipomwona tena.

Bassi nikarejea hali yangu ileile ya kwanza, nikakaa kitambo kidogo hivi. Nikamsikia mtu, akanipa salaam, nikamwitikia. Akaniuliza, wanijua mimi? Nikamwambia, sikujui. Akaniambia, mimi ni nduguye nyoka mweupe, naswi watu watatu, kulla mmoja amekutendea awezalo, bassi na mimi nimekuja kukutendea niwezalo. Akaniambia, tumekaribia sasa mji wa Nuhás, tumefika, ni ile unayoiona pale.

Nikamwambia, nimeiona, nitaiingiaje kule? Akatoa upanga akanipa, akaniambia, chukua huu upanga. Na upanga ule umeandikiwa talassimu, wote. Nikaushika upanga. Nikamwuliza, njia i wapi ya kuingilia ndani? Nayo ule mji wa Nuhás, mtu mmoja hawezi kufungua mlango, wala wawili, wala watatu, na mlango wake umefungwa, nitapitia wapi mimi? Akaniambia, fuata mto wa maji, na mto huu unaingia ndani ya mji wa Nuhás.

Nikafuata mto ule na upanga wangu mimechukua mkononi. Nikafuata mto, hatta nikaingia ndani ya mji. Nikiingia, nimeona mambo ya miujiza, kulla laoni ya vitu nikaviona, nivijuavyo nisiovijua. Nikaenenda na upanga wangu mkononi, haingia katika mji, hatembea katika mji. Nami haona nao, lakini wao hawanioni, kwa sababu ya upanga wangu ilioandikiwa na talássim.

Nikazunguka hatta nikamwona manamke, mke wangu. Nilipomwona, marra nikamtambua, naye akanitambua, nikamjongelea, tukaonana tukaulizana khabari. Nika-