Page:Swahili tales.djvu/196

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
176
MOHAMMADI MTEPETEVU.

pete mno ufunguo, fungua uingie ndani, utaona sanduku kubwa limejaa katika ghala, juu ya sanduku pana sufuria, na juu ya sufuria pana tassa, na ndani ya tassa mna maji, na mkono wa kushoto wako pana jogoo mwekundu, na mkono wa kulia wako pana kisu kimeandikwa talássim. Bassi twaa kisu kile, unchinje jogoo juu ya sanduku, ukaisha kumchinja utoe maji yale ndani ya tassa ile, uoshee kisu. Bassi ukaisha fanya amri hiyo, utaona sanduku itafunguka, na ndani ya sanduku utaona khazina, na khazina hiyo mwenyewe haijui Sherifu, nawe ukiisha ipata utastarehe. Kwani mimi Mwenyi ezi Muungu amenifanya nyani kuja kuwa iftahi yako. Nawe utastarehe nafsi yako, nami ntakwenda zangu. Lakini sharti ufanyize kama kayo, na usipofanyiza, hutaona mema illa utaona mabaya tu.

Nikamwambia, nitafanya kama haya uliyoniambia.

Nikaenda nikaingia nyumbani kama aliyoniagiza kufanya, nikafanya. Katika kufungua mlango kule nikamsikia yule kijana binti ya Sherifu, mke wangu, niliyo'moa, akanena; Amekwisha nichukua Jini. Hatta nilipokwisha ingia nilipotoka, nikaenda chumbani kwa mke wangu, hako. Jini amekwisha mchukua. Bassi nikawa hali yangu kama mtu mwenyi wazimo.

Khabari akaipata babaye Sherifu, marra akaja nyumbani, akija kwa kulia na kujipiga makonde, na kupasua nguo. Hatta akifika pale, akaniambia, haya ndio aliyoyataka, kwani mimi Jini nalimwona zamani kutaka kuniibia mwanangu, nikamfunga kwa haya matalassimu, uliokuja kuyafungua. Nayo yale ni madawa yaliomfunga hatta geuka nyani. Na wewe umekuja umemfungua, kunipotezea mwanangu. Bassi na sasa ni kheiri uniondokee