Page:Swahili tales.djvu/194

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
174
MOHAMMADI MTEPETEVU.

kuja kuposa binti yake. Atakwambia, huna ásili wala fásili. Mwambia, ásili ni dinari elfu, na fásili dinari elfu. Bassi ukamwambie na kulla utakalo, na ukiisha mpa ásili na fásili, atakubali, lakini atakuihtajia mali mengi. Atakachotaka cho chote mpe, wala usione choyo, na ukiisha oa, mali yako hayo utakayoyatoa utajilipa na zayidi. Tukaagana nikalala.

Hatta kulipokucha nikafanya kama alioniambia. Nikafanya uzuri mimi, na watumwa wangu, na bághala yangu, nikapanda, nikaenenda hatta katika soko ile, nikaenda nikamwona Sherifu, nikampa salaam, akaniitikia. Nikamwambia, jongolea, nikamweleza khabari yangu, akanijibu maneno kama yale aliyonena nyani. Akanambia, huna ásili wala huna fásili. Nikampa dinari elfain, elfu za ásili, na elfu za fásili. Akakubali, akanipa shuruti zake.

Akaniambia, dinari elfu mahari, na dinari elfu nguo, na dinari elfu kilemba changu. Nikampa dinari khamsi elafu, nikatoa na dinari elfu, nikawapa waliohuthuria, nikaoa. Nilipokwisha oa nikaenda nikamwambia nyani kama nimekwisha kuoa.

Akaniambia ulimwengu wako utakufanikia, bassi katake saa ya kuingilia nyumbani, nina khabari nataka kuja kukupa. Nikaenda nikataka saa ya kuingilia nyumbani, nikaisha nikamwambia, nimepata.

Bassi akaniambia, usiku utakayoingia nyumbani ukipita mlango wa kwanza, tezama katika behewa, utaona mlango upande wa shoto, pana na pete katika mlango ule, katika