Page:Swahili tales.djvu/192

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
172
MOHAMMADI MTEPETEVU.

katika kinwa chake, akaja hatta nilipo, akaniwekea mbele yangu, nikaushika mfuko ule nikaufungua, nikatazama ndani mna thahabu, nikazimimina thahabu ile mashkhas, nikahasibu khamsi mia, nikazitoa nikaziweka, nikakaa hatta subui. Zamani nilipokula akaja hula sote, nikakaa hali hiyo, hutoka assubui, hukarudi akatoa mfuko mashkhas. Hatta siku nyingi zikapita.

Hatta siku hiyo usiku, nimelala katika órafa yangu, yule nyani akanijilia, akampa salamu, nikamwitikia. Lakini moyo wangu nimefazaika, nikafanya khofu sana, kwa sababu kuona nyani kusema. Akaniambia, Mohammadi, usifanye khofu, mimi, Mwenyi ezi Muungu amenijalia kuwa nyani, lakini si nyani mimi, mimi ni Jini il Maradi. Mwenyi ezi Muungu amenijalia kuwa iftahi yako, kukutoa katika umaskini, nawe usifanye khofu. Nna maneno nataka kukwambia. Wewe walikuwa mtu mmoja fukara, huna mbele huna nyuma. Mwenyi ezi Muungu amefanya mimi kunigeuza kuwa nyani kwa ndio sababu yako, ya kupatia mali. Na sasa ulionayo hayajawa mali, kwani huna mke. Bassi nimekupatia manamke, nataka nikuoze, na ukipata mke huyu, utastarehe nafsi yako, na mali utapata zayidi.

Nikamwuliza, ni yupi mke huyo? Akaniambia, kesho assubui fanya uzuri, uvae nguo borabora, na bághala yako utandike matandiko ya thahabu, ufuatane na vitwana walio wema miongoni mwa watumwa wako, uenende hatta soko il aláf. Wenende hatta baraza ya fullani, utamwona Sherifu amevaa nguo za kitaowa. Bassi mkaribia huyu, mpe salamu, mweleza khabari yako ya kutaka mke, ya