Page:Swahili tales.djvu/190

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
170
MOHAMMADI MTEPETEVU.

ya kunithihaki. Ni kitu gani nilichompa hatta kuniletea makasha haya? Mimi nalimpa dirliamu tano, na thamani ya dirhamu tano ni huyu kima alioniletea. Bassi, hana haja ya kunifanya thihaka, mimi maskini ya Muungu.

Na yule aliopeleka amana ile, makasha, akaniambia, hakuthihaki, walaye, si mtu wa kukufanyizia thihaka. Na yee mwenyewe atakuja sasa hivi.

Tusijaisha kusema maneno yale, marra nasikia—hodi! Nikimtazama, ni Sheikh Abalmathfár nikaondoka mwenyewe nikakaa kitako, nikamkaribisha.

Akakaa kitako akanieleza khabari yake, toka mwanzo hatta mwisho iliowapata tangu kusafiri kwao. Akaniambia, na haya makasha ndiyo fayida yako, na viliomo ndani; na huyu kima, ndio ras il mali yako. Akanitaka rathi sana, akaniambia, mimi si mtu wa kukufanyizia thihaka wewe. Tukaagana, akatoka akaenda zake.

Tukafungua kasha, tukatazama tukaona mali mengi. Mama yangu akaniambia, walikuwa mvivu, hukuona kitu na sasa Mwenyi ezi Muungu amekupa kheri. Bassi ondoka ukatafute nyumba ilio njema, ukae. Bassi nikaondoka nikaenda nikatafuta nyumba, nikanunua nyumba ilio njema, nikanunua na pambo la nyumba, nikanunua na watumwa wa nyumba, vijakazi, na wazalia, na Habashi, nikatia katika nyumba yangu. Na killa kilichoihtajia nyumba, nikanunua nikatia. Nikanunua na bithaa, nikafanya duka.

Na mimi mwenyewe hukaa dukani, na nyani wangu hukaa nami pamoja. Hatta assubui nyani akaondoka, akaenda, harudi illa jioni, na anapokuja huchukua mfuko