Page:Swahili tales.djvu/180

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
160
MOHAMMADI MTEPETEVU.

Wakaenda wakafika kwa Khalifa, wakatoa salamu mbele yake Khalifa. Naye Khalifa amekaa, na mawaziri wake pale. Akamkaribisha. Akaanguka chini ya miguu yake Khalifa yule mtepetevu. Akamwambia, nataka msamaha kwako, nna maneno nataka kwambia. Akamwambia, sema. Bassi akainua uso wake, akatazama juu. Akatikiza midomo yake, zikapasuka juu ya nyumba, yakatoka kama majumba, na bustani, na miti ndani ya bustani, na miti ile majani yake ya lulu, na matunda yake ya marijani.

Khalifa akastaajabu mno. Akamwuliza, Mali haya umepata wapi wee? Nawe hatukufahamu ela Mohammadi mtepetevu, na baba yako alikuwa muumishi katika hamami. Bassi ilikuwaje hatta ukapata mambo haya weye? Akamjibu, akamwambia, ukiniamuru ntakupa hadithi yangu. Na haya pia sikukuletea kwa kuogopa, lakini nimetazama haya hayafai ela kwako weye mfalme. Bassi kama wataka nikupe hadithi yangu, ntakwambia. Mfalme akampa amri, akamwambia, lete hadithi yako.

Akamwambia, zamani za kwanza nilipokuwa mdogo, na baba yangu alipokufa, nilikuwa mvivu sana, hatta chakula akinilisha mama yangu. Na nijapolala, siwezi kugeuka ubavu wa pili, sharti aje mama anigeuze. Ikawa mama akienda kuomba, akipata kitu akinilisha. Nikakaa hali hiyo miaka khamstashara katika uvivu.

Hatta siku moja akaenda mama, akaenda akaomba, akapata dirhamu tano, akinijia kule nyumbani kwangu nilipolala, akanambia, leo nimekwenda omba, nimepata hizi dirhamu tano, bassi, twaa hizi dirhamu tano umpelekee Sheikh Abalmathfár. Naye Sheikh anasafiri,