Page:Swahili tales.djvu/178

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
158
MOHAMMADI MTEPETEVU.

Akamwambia, ningoje siku ya leo ishi kwani nataka bághala wa kupakia zawadi zangu nitakazo kumpelekea kalifa. Akamwambia, nimekupa ruksa ya leo. Akafanya shughuli zake, mchana kutwa. Siku ile ikawa kustarehe hatta jua likachwa. Akaingia katika hamami waziri yule Masruri Sayafi. Alipotoka akapelekewa kama zile za kwanza akavaa. Na killa nguo anazovua hukunjwa zikatiwa ndani ya kasha na mfuko wa dinari khamsi mia. Na nguo hizo na fetha hizo zake mwenyewe Masruri Sayafi.

Wakakaa hatta assubui wakafanya safari yao. Wakaletwa bághala ároba mia, mabághala hao kupakia haja zake Mohammadi mtepetevu. Wakapakia, akaamrisha kutandikiwa bághala wake wawili, kwa seruji ya thahabu, na lijamu zake za thahabu, na vigwe vyake vya hariri. Mmoja akapanda yule mwenyewe Mohammadi mtepetevu, na mmoja akapanda yule waziri Masruri Sayafi. Na liwali Mohammadi Zabidi, wakaingia katika safari, kusafiri kwenenda kwa Kalifa, inchi ya Baghdadi. Wakasafiri jeshi kuu. Wakaenda njiani.

Jua likichwa wakafanya khema zao, wakalala. Na khema ya Mohammadi mtepetevu, khema yake hariri, na miti yake ya uudi, wakalala, yeye na waziri Masruri Sayafi.

Assubui wakaamka wakatoa vyakula vyao na vinywa vyao, wakala wakinywa. Wakaisha wakatandikwa nyama zao, wakapanda. Ikawa hali hiyo, jua likichwa wakalala, na usiku ukicha wakaenenda. Na katika safari mle, yule waziri Masruri Sayafi akawaza ndani ya moyo wake, akanena, Mimi nitakapofika kwa Kalifa nitamwambia, amuulize sababu yake ya kupatia mali mengi hivi. Nami namfahamu babaye, alikuwa muumishi katika hamami.