Page:Swahili tales.djvu/156

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
136
SULTANI DARAI.

rudi hali yake kama kwanza, watoto wakamzomea, Huu! huu! Amekwenda wapi huyu? Atoka wapi huyu? Siye twalinena amekufa, kumbe mzima bado?

Na yule mwanamke akajikalia na mali yake kule, yeye na babaye, na nduguye, na jamaa yake, raha mustarehe.

Na yule babangu mimi, maskini, akawa kazi yake ileile, kama kwanza, ya kupekua chini, na hupata punje za mtama akitafuna.

Ikiwa njema, njema yetu wote, na ikiwa mbaya, ya mwenyewe mosi, aliofanya hadithi hii.