Page:Swahili tales.djvu/154

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
134
SULTANI DARAI.

waliomo wakalia sana, kwa sababu ya uchungu wa yule paa. Akimtoa Sultani paa nje. Wakimchukua.

Na wale watu watatu wakarudi wakaenda kumjibu bibi. Wakamwambia, Babako amekuja na wangwana bora walio katika mji, nao walikuja, nao wamechukua paa, wamekwenda zao. Wamwambia bibi, Si kilio kilichokuwako ndani ya kisima? Watu wote walilia kama siku aliokufa mamaye Sultani.

Akawaambia, na mimi tokea siku aliokufa paa yule, sijala chakula, wala sijanywa maji, sijanena, wala sijacheka.

Yule babaye akaenda akazika paa. Akamfanyizia matanga makuu sana, akamfanyizia na msiba mkuu sana katika mji.

Hatta baada ya kwisha msiba, yule mwanamke amelala na mumewe usiku, katika usingizi yule mwanamke akiota, yuko kwa babaye, na yule wakati anaota ule umekuwa ussubui, akafunua macho yule mwanamke, anajiona katika mji wa babaye, na nyumba ileile aliokuwa nayo kule.

Yule mwanamume akiota kama yuko pale jaani, akapekua. Na yule wakati anaota, limekuwa jua wakati wa saa ya pili, nao ndio wakati anaokwenda kupekua, killa siku. Hatta alipofunua macho, Sultani Darai akaona mkono wake u katika jaa, unapekua. Akasangaa, Ah! nimekuja na nani huku? Akatazama ya mini wa shemali haoni kitu. Akatazama mbele, aona giza, na akitazama nyuma aona vumbi. Marra pale watoto wakipita, ame-