Page:Swahili tales.djvu/150

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
130
SULTANI DARAI.

yeye apenda kutia katika macho akuweke, lakini hathubutu, hana amri mwanamke, nami nimepewa kukuletea maziwa haya, na mchele huu, na nguo ya kujifunika, na mto huu, na killa unachotaka, nambie wala usinifiche, anakwambia bibi, na kama wataka kwenda kwa babaye, atakupa watu wakupeleke, wakuchukue polepole, na huko utakwenda fanywa dawa sana utatazamwa sana, una heshima nyingi huko sana. Bassi nijibu, nikamwambie bibi.

Marra paa akafa.

Alipokwisha kufa, nyumba nzima watu wakalia, watumwa kwa wangwana, mkubwa kwa mdogo, mke kwa mume.

Akaondoka yule Sultani Darai, akawaambia, Mnalia nini, mnalia nini? Akawaambia, mnalilia paa kama naliokufa mimi. Yule aliokufa ni paa tu, thamani yake themuni.

Yule mkewe akamwambia, Bwana twalimwona paa hatta kukuona wewe. Paa ndio aliokuja kunitaka kwa baba yangu, paa ndio alionichukua kwa baba yangu, paa ndio aliopewa mimi kwa baba yangu.

Wakamwambia, Sisi hapa hatukukuona wewe, twalimwona paa ndio aliokuja, akakuta taabu hapa, ndio aliokuja, akakuta nafasi hapa. Bassi na mtu yule kuondoka katika huu ulimwengu sisi twalilia yetu, hatumlilii paa.

Wakamwambia, Paa amekufanya vema vingi, na vikiwa vema na viwe kama hivi, wala visizidi, na anenayo viko vema vizidio hivi mtu huyu mkanye tena mwongo. Ee bassi, sisi tusiokutenda vema, utafanyaje? Yule paa aliotenda vema vyote, wala hukumjua kwa kheri, wala