Page:Swahili tales.djvu/148

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
128
SULTANI DARAI.

kuwa msimamizi wako katika nyumba. Tena paa yule, bwana wangu, mume wangu, Sheki langu, Eh! Sialtani Darai, mimi nalinena una akili nyingi, kumbe huna akili hatta kidogo, bwana, kumi hatta moja kwako halipatikani jema. Bwana, ukuu si pembe kama mtu ataota, ukuu shuti astahamili, na huyu mkuu ni jaa, killa mwenyi taka yake humwaga, kwani hili jaa halina mtu mmoja, halina tajiri, wala halina Sultani, wala halina Kathi, wala halina maskini, wala halina mkubwa, wala halina mdogo, wala halina mke, wala mume.

Akamwambia, wewe una wazimu mke wangu. Akamwambia, Maneno yako yote hayo, ni nguo yangu ya pili ya kujitanda.

Bassi bwana, mzee analia, haliki hatafuniki.

Akashuka mzee hatta akifika kwa paa, akamkuta paa, anatapika, akiondoka, akimdaka, akimpakata, paa na yule mzee wakalia sana.

Akaondoka yule bibi darini, akaiba maziwa, akaiba na mchele kidogo, akatwaa na mjakazi, akamwambia, twaa ukampikie paa chini mpe, akamwambia, twaa na nguo hii, ukampe ya kujifunika, na mto huu kampe, aulalie, na killa anachotaka, na anachotamani, na amtume mtu aje kwangu, asimwambie bwana wake, kwani bwana wake hatampa. Atapotaka hapa, nimpe watu wampeleke kwa baba yangu, akafanywe dawa, atatazamwa sana huko, nitampeleka.

Akashuka yule mjakazi hatta chini, akamwambia paa, Salaam sana bibi, haya si yake, ni ya bwana wako,