Page:Swahili tales.djvu/146

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
126
SULTANI DARAI.

Akaambiwa bwana, na huku mzee analia. Akamwambia, Bwana, paa hawezi sana, twamwona kufa ku karibu kuliko kuwa mzima.

Akamwambia, nimekwambia usiniuthi.

Mkewe akamwambia, Ee bwana, hushuki ukaenda kumtazama paa wako, hushuki kumtazama kiatu chako, hushuki kumtazama mboni yako wa jicho, hushuki kwenda kumtazama karani wako, hushuki kumtazama msimamizi wako? Na kama hutaki kushuka wewe, nache mimi nikamtazame. Bassi kwako kumi hatta moja halipatikani jema.

Akamwambia, Enenda kamwambia paa, kama watu hufa marra moja, yeye na afe marra kumi na moja.

Mke akamwambia, Ah! bwana, amekutenda nini paa, amekukosa nini paa? Maneno haya hamwambii mtu illa adui yake, asiopenda kuona. Ehe, weye na paa, bwana, mna wadui gani? Bwana, mambo yako unaomtenda si mema, wala wewe kuyafanya haya, wala kumfanyizia paa. Watu wakisikia watakucheka, kwani huyu paa si mdogo, paa amependwa tokea wangwana hatta na watumwa, paa amependwa na wadogo hatta nao wakubwa, paa amependwa na wake hatta na waume. Bassi wewe bwana, kwani ukamchukia paa huyu, wala siyo maungwana. Mngwana akitendwa jema kulipa jema. Mngwana hatendwi jema akalipa maovu, sicho kiungwana. Bassi kwako mambo kumi hatta moja, halipatikani jema kwako. Kama paa huyu wewe humpendi kwa uzuri, mpende kwa kunena, kama humpendi kwa kunena, mpende kwa sababu kuwa mtu wako, unamtuma hapa na hapa, kama humpendi kwa hilo, mpende kwa sababu anavyojua heshima za watu, kama humpendi kwa hayo, mpende kwa