Page:Swahili tales.djvu/144

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
124
SULTANI DARAI.

amekuja mtu, paa hawezi, marra amekuja mtu, paa hataki kula, na potelea mbali, akitaka kula na ule, hakutaka, na apotelee mbali. Mama yangu amekufa, na baba yangu amekufa, nami ninakula na kunywa, sembuse yule paa mmoja, naliomnunua kwa themuni, atakuwa akinipanza na kunishusha? Nenda kamwambia paa ataadabu.

Akishuka yule mzee, huku anatoka damu, huku anatoka uzaha. Akaenda hatta akimwona paa, yule mzee akamkumbatia paa, akampakata, akamwambia, Mwanangu, mema yako walioyatenda yamepotea, yaliosalia stahamili.

Akamwambia, Mama, matumbo yangu yamejaa, na ulimi wangu mzito, na macho yamefanya kiwi, kwa haya ninayoyasikia. Wakalia sana wote wawili, paa na mzee.

Akamwambia, Mama, mimi ntakufa, kwani roho yangu umejaa ghathabu sana, imejaa na uchungu sana, na uso wangu nimetahayari kumtenda bwana wangu vema, kunilipa maovu.

Akamwambia, Ahh! mwanangu, sina la kunena.

Akamwambia, Mama, mali yaliomo katika nyumba hii mimi paa mmoja nnakula gani? Killa siku angenipikia nussu kibaba, naye hangepungukiwa na kitu bwana wangu. Nimesumbuka mimi kuchuma, mimi kuugua, kwambiwa nikatwaliwe felefele, asiokula frasi, nifanyiziwe uji mimi? Wazee walinena, mtenda mema cha nina.

Akamwambia, Enenda baada juu kamwambia bwana, paa hawezi sana, mwambia, kumwona kwetu, twamwona kufa ku karibu kuliko hayi.

Akaenda hatta darini, akamwona bwana, atafuna 'mua.