Page:Swahili tales.djvu/140

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
120
SULTANI DARAI.

Paa akanena, Ha! mimi ndio kufanyiwa uji huyo, akakwambia yeye bwana?

Bassi naweza kukwambia uwongo, baba? Akaniambia mwenyewe bwana na mkewe yuko, hatta mkewe akigombana naye bwana kwani kumfanyia hivyo paa, na bibi akatukanwa kwa sababu wewe kukugombea.

Paa akanena, Wazee walinena, mtenda mema cha nina, nami nimemtenda zema, nami nimepata haya walionena wazee.

Akamwambia, Mama, enenda tena juu kwa bwana, usichoke kwa haya ninayokuagiza, ukamwambie bwana,—paa hawezi sana, na ule ulionambia mtama kumfanyizia uji, hakunywa.

Akaenda yule mzee, akamkuta bwana na bibi, wamekaa katika dirisha, wanakunywa kahawa. Alipotupa macho yule bwana nyuma yake, amwona yule kizee. Akamwambia, Una nini wee kizee? Akamwambia, Nimetumwa bwana na paa, ule mtama walioniagiza kumfanyizia uji; hakunywa, naye hawezi sana paa.

Akamwambia, Eee chúb! zuia ulimi wako, uzuie na miguu yako, ufumbe na macho yako, uzibe na masikio yako kwa nta, akikwambia paa, panda juu, mwambia miguu yangu haiwezi kupanda darajani, imekunjika. Akikwambia sikia, mwambia masikio yangu hayasikii maneno yako, yamezibwa na nta, akikwambia, nitazame, mwambia, macho yangu yametiwa vijamanda kama anavyofungwa ngamia, akikwambia njoo tunene, mwambia, ulimi wangu nimetiwa kulabu, hauwezi kunena nawe.

Yule mzee akasangaa, kwa sababu ya maneno yale kwambiwa, na sababu alipomwona paa kuja katika mji ule akaja kuuza roho kununua mali, lakini roho akapata, na mali akapata, na leo anavyomwona heshima yake hana