Page:Swahili tales.djvu/134

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
114
SULTANI DARAI.

paa wangu, je! mtumwa wangu, je! kiatu changu! nyumba hii umepataje? Mji huu mwenyewe nani? Nyumba hii mwenyewe nani? Ao nyumba hii unapanga, ao nyumba hii umenunua, ao mji huu umepewa, ao mji huu hamna watu kumi hatta moja. Bassi, mama, mambo haya, mambo gani? Zema zote nnazomtenda bwana, naye hatta siku moja hajanitenda jambo jema, alijua mtu aliokuja naye hapa, nyumba hii si yake, wala inchi hii si yake, tokea alipozaliwa hatta leo hakupata kuiona nyumba kama hii, wala hakupata kuuona mji kama huu. Bassi yeye anga haniiti kwa thikaka, akaniuliza. Lakini watu wamenena, hakuna wema watu mtenda zema cha nina, na wazee walinena ukitaka kumtenda mtu vema, simtende mema matupu, mtende na mabaya, ndipo mtakapopatana wewe naye. Akamwambia, bassi mama, nimekwisha, nataka kutazama fathili nalivyomtenda bwana wangu, nami atanifathili. Akamwambia, Vema baba, wakalala.

Hatta ussubui walipokucha, paa akaugua tumbo na homa na miguu yote kumwuma. Akamwambia, mama! Akamwitika, Labeka, baba. Akamwambia, Enenda kamwambia bwana darini, paa hawezi sana. Akamwambia, vema, baba, na akiniuliza, hawezi nini, nimwambieje? Mwambia, Maungo yote yaniuma sana sina pahali pamoja pasiponiuma.

Akaenda yule mzee hatta darini. Akamkuta bibi na bwana wamekaa katika kitanda cha mawe ya marmari, na godoro ya mdarahani, na takia huku na huku, wakati hutafuna tambuu, mke na mume.

Wakamwuza, Je! kizee, umekuja taka nini? Akamwambia, kwambia bwana, yule paa hawezi. Yule mwa-