Page:Swahili tales.djvu/130

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
110
SULTANI DARAI.

sikumjua kama ndiye bwana wetu. Akamwambia, nawe, bwana, niwie rathi sana, mtumwa wako, sina habari kama wewe ndio bwana wetu. Akamwambia, ni rathi.

Akaondoka pale, ukifunguliwa mwango, tokea chini hatta juu, na vyumba vyote, na ghala zote, ya mini wa shemali. Akaingia yule kijana, akawaambia, wafungueni hawa watu waliofungwa. Wangine na wafagie, wangine watandike vitanda, na wangine wapike, na wangine wateke maji, na wangine watoke nje wapate kwenda kumtwaa bibi.

Yule Sultani Darai akaona nyumba ile mzuri sana, akaona, vitanda vizuri mno, akaliona pambo la nyumba, hakupata kuliona, wala hakupata kulisikia pambo kama lile. Roho yake ikafurahi sana, moyo wake ukaona, kama mtu alioletwa habari na Muungu, kama wewe umekwenda ingia peponi, kwa roho yake yalivyofurahi.

Wakaenda watu kule, wakaenda wakamchukua bibi na wale wangwana waliokuja, na wale watumwa wao waliokuja nao, na mwenyewe pambele, wakaja nao hatta wakafika nyumbani. Akawaambia, Karibuni wangwana, piteni wangwana. Akawaambia, karibuni jamaa, piteni ndani jamaa zangu. Waanawake mwende darini. Walipokwenda wangwana wakapita, akawaambia, na hawa frasi, waliokuja na wangwana, na wapelekwe uani, wakakaa.

Bassi wakaenda wakafanya vyakula vingi sana, wakafanyiziwa wali mzuri sana, wakala, wangwana kwa watumwa, kwa killa mtu, akashibia nafsi yake. Wale waanaake waliokuja, wakamwambia, Ah! paa wee, eh! baba wee, sisi tumeona majumba, sisi tumeona watu, sisi tumesikia mambo. Wallakini nyumba hii, na wewe ginsi ulivyo, hatukupata kuona wala hatukupata kusikia, na mwenyi kutaka kuona, na one nyumba kama hii, asizidi