Page:Swahili tales.djvu/128

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
108
SULTANI DARAI.

ndoka. Akawaambia, Wajoli! Wajoli! Wakamwitika, Labeka baba. Ondokeni, nawe uso. Wakamwambia, tumeondoka, baba. Waandikiwa chakula, wangwana kwa watumwa, wakubwa kwa wadogo. Haya, wangwana, fungueni kinywa. Akaenda akawaambia, haya wajoli, fungueni kinywa. Watu wakala hatta wakashiba. Walipokwisha kula hakujapambauka bado. Haya, wangwana, twendezetuni.

Wakaondoka wakaenda zao. Wakaenda hatta alipokoma jua vitwani paa akaona, na wale wangwana waliofuatana nao wakaona dalili ya jumba mbele yao. Wakamwita, Paa! Akaitika, Labeka, bibi zangu. Wakamwambia, mbele yetu twaona kama dalili ya nyumba. Akawaambia, Oh! bibi, bassi huu, si huu mji wetu? Ndio nyumba ya Sultani Darai.

Waanaake wakafurahi sana, na wale watumwa wakafurahi sana. Wakaenda hatta yalipokoma muda wa saa mbili, wakawasili katika mwango wa mji.

Akawaambia paa, Wangwana kaeni hapa, wangwana kwa watumwa, wake kwa waume, niacheni mimi na Sultani Darai twende nyumbani. Wakamwambia, Vema. Akaondoka paa na bwana wake, hatta wakiwasili katika nyumba.

Yule kizee aliyo katika nyumba alipomwona paa, anakuja, aliruka na kigelegele na hoihoi, na kuranda, na kwenda mbio hatta akawasili katika miguu ya paa. Akimchukua, aki'mbusu. Paa akamwambia mzee, Nache, wa kuchukuliwa ni huyu bwana wetu, wa kubusiwa ni huyu bwana wetu, kwani mimi nikiisha fuatana na bwana njia moja, heshima za kwanza apewe bwana, bassi ndio nikapewe mimi. Akamwambia niwie rathi, baba, sana,