Page:Swahili tales.djvu/126

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
106
SULTANI DARAI.

Wangwana wale wakampenda yule paa mapenzi yalio bora yasiokuwa na kifani. Na wale watumwa wao walimwona yule paa kamma mboni zao za macho, gissi wanavyompenda kwa ginsi walivyomwona tamu.

Akawauliza, wangwana mmeshiba? Wakamwambia, hapa tulipo hatta pumuzi twajiona kuwa ndogo nasi. Akawauliza, ewe wajoli wangu, wake kwa waume, anao njaa asinifiche. Wakamwambia, sisi hatuna njaa. Akawaambia, Haya wangwana, twendezetuni. Wakaondoka, wakaenda hatta yalipokoma saa edashara, akawaambia, wangwana hakuna mwendo wa usiku. Akawaambia, na tukae. Wakakaa kitako. Kikaletwa chakula, wakala, wangwana na watumwa, wakashiba, wangwana na watumwa, wakafurahi, wangwana kwa watumwa, kwa zile heshima walizozipata kwa paa, wakamwona yeye bora angawa paa, wakamwona zayidi kuliko bwana wake Sultani Darai. Akaanza toka mwanzo hatta mwisho, mngwana kwa mahali pake, na mtumwa kwa pahali pake, na mkubwa kwa pahali pake, na mdogo kwa pahali pake. Bassi akarudi, akaja akalala hatta jogoo la kwanza lalipowika. Akaondoka, akamwambia bwana wake. Akamwambia, Bwana! Akamwambia, Labeka baba, akaitika, labeka, azizi wangu, labeka mvika nguo yangu, nambie ulilo nalo, baba. Akamwambia, Hapo tulipo na nyumba tunaokwenda nnavyoaza, napenda nafsi yangu tuondoke na mapema hapa. Akamwambia, Vema. Bassi mimi nitaamshe wangwana wafungue kinywa na mapema, tupate kwenda zetu. Akamwambia, halitupata athuuri tutauona mji. Akamwambia, Vema.

Akawaamsha, Wangwana! Wangwana! Wakamwitika, labeka. Akawaambia, Ondokeni na nawe uso. Wakao-