Page:Swahili tales.djvu/124

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
104
SULTANI DARAI.

sana, tokea lalikwanza kutoka jua, hatta kuchwa kwake hukupata kupumzika hatta marra moja, hatta huu usiku. Akamwambia, tafathali nawe lala. Nawe usikasirike, baba, mkuu ni jaa, mtukuzi ni atukuaye, asiotukua si mtukuzi. Akamwambia, kweli. Wakalala.

Hatta ussubui kabla hakujapambauka vema, akaamsha wangwana. Wangwana, Wangwana, amkeni. Wajoli, Wajoli, Wajoli, amkeni. Wangwana naweni uso, na wajoli wangu naweni uso.

Akawaambia, njooni wangwana mfungue kinywa, na wajoli, wajoli, njooni mfungue kinywa, tupate kimbia jua. Wakaondoka wale wangwana wakala vyakula vema, wakafurahi, roho zao hatta watumwa. Na wote waliopo, watumwa kwa wangwana wakampenda yule paa kuliko Sultani Darai.

Wakiisha, wakaondoka. Je! Wangwana mmeshiba? Wakamwambia, tumeshiba. Wakamwambia, sisi ni wangwana, hatta kama hatukula chakula hichi, kwa heshima zako na kwa mambo yako sisi pekeyetu hushiba. Akamwambia, ahsánt. Akauliza, Je! jamaa zangu mmeshiba? Wakamwambia, Hapo tulipo sisi hatta ukope twaonea mzito kutia tumboni mwetu, kwa ginsi tulivyoshiba.

Akamwambia, Haya tusafiri sasa. Wakaenda hatta lalipokoma jua vitwani, wakatua. Na tupumzike hapa tunywe maji, tule chakula. Bassi kikaja chakula, wakala, wangwana kwa watumwa, wakashiba, wangwana kwa watumwa, wakafurahi, wangwana kwa watumwa.