Page:Swahili tales.djvu/120

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
100
SULTANI DARAI.

akanena, bwana wangu atafurahiwa kwa hayo naliyomtendea, kwani bwana wangu akiwa na nyumba hii, naye mtu aliyekuwa mbali, atakuwa kama aliozaliwa marra ya pili, ginsi atakavyojiona mzuri.

Akakaa nyumbani akizumgumza na kizee yule, hatta baada ya siku ya tatu, akaenda zake.

Akaenda hatta akawasili katika ule mji, alioko bwana wake. Sultani aliposikia yule paa amekuja, alifurahi sana, akaona kama mtu alioshushiwa jaha. Hatta alipopata habari bwana wake ndani aliko, akaona nafsi yake kama mtu alioyona leilat al kadri. Bassi akaondoka aka'mbusu sana. Baba yangu, umekawia, umeniacha sikitiko, nimekaa kukumbuka, siwezi kula, siwezi kunywa, siwezi kucheka, moyo wangu haukuona tabassamu kwa jawabu liwe lote, na sababu kukumbuka wewe.

Akamwambia, mimi mzima, na nitokako kwema, nami napenda baada ya siku nne, kutukua mkewo, twende zetu kwetu. Akamwambia, Ni ihtiari yako, ni lile unambialo ndilo nitafuata. Bassi, akamwambia, mimi nnakwenda kwa mkwewo, hamkhubiri habari hizi. Akamwambia, Enenda.

Akaenda hatta barazani, akamwambia, Bwana nimekuja kwako. Akamwambia, Bashiri kheiri, nambie uliyojia. Akamwambia, Nimekuja, nimetumwa na bwana kuja kukwambia, baada ya siku nne, atakwenda zake, yeye na mkewe, nawe nimekupasha habari. Akamwambia, mimi sipendi kuondoka upesi, kwani hatujakaa sana, mimi na Sultani Darai, wala hatujazumgumza sana, mimi naye, tokea alipokuja hatta leo siku arobatashara, hatujapata kukaa mimi naye tukazumgumza, wala hatujapata kupanda