Page:Swahili tales.djvu/116

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
96
SULTANI DARAI.

akaingia katika sufuria zake kula, hatta alipokwisha kula, akaja hatta akafika pale mlangoni. Akasikia harufu ya kitu chingine kiwamo ndani. Akamwita, wee kizee, mbona leo nasikia harufu nyingine, humo ndani? Akamwambia, bwana, mimi hapa pekeyangu, nimekaa siku nyingi, sikupata kujisinga, leo nimejisinga, bassi ndio unaposikia harufu hii, unanena ndio kuna kitu kingine ndani. Kitatoka wapi kitu hapa, Bwana?

Na yule paa ameutoa upanga amekaa tayari. Yule nyoka akitia kitwa ndani, paa upanga umemtoka, akamkata kitwa, yule nyoka asijue kama amekatwa kitwa. Akipenyeza cha pili, yule paa umemtoka upanga, akamkata kitwa cha pili. Yule nyoka akainua kitwa akamwambia, umekuja nani katika nyumba yangu kunikunakuna? Akikitia kitwa cha tatu kutaka kuingia ndani, paa umemtoka upanga, akimkata kitwa cha tatu.

Hatta alipotimiza vitwa sita, ghathabu za nyoka, akajiacha mapindi, yeye paa na yule kizee wasionane kwa vumbi. Hatta alipotia kitwa cha saba, alipokitia mwangoni, paa akamwambia, Leo ndio mauti yako, akamwambia, miti pia umepanda huu ndio mparamuzi. Akainua kitwa kuingia nyoka ndani, paa upanga umemtoka, akamkata kitwa cha saba. Paa akianguka akizimia.

Bibi yule kizee, akapiga kigelegele, akapiga na hoihoi, akajiona mwili wake na macho yake, na roho yake, na nguvu zake ni kama mtoto wa miaka tissa, naye ni mtu wa miaka khamsi u sabwini. Akaondoka mbio yule kizee, akamchukua yule paa, na yule paa amezimia, akamtia maji, na kumpepea, na ku'mweka pahali palipokabili baridi, hatta paa akatweta, hatta paa akaenda