Page:Swahili tales.djvu/114

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
94
SULTANI DARAI.

huenda zake, haji illa kwa siku ya pili, wakati uleule jua vitwani. Bassi uta'mweza api, baba, nyoka huyu? Naye ana vitwa saba, hawaku'mweza kindakindaki wafalme wa nyuki, uta'mweza wewe baba?

Akamwambia, mama, ona ulicho nacho usione usichokuwa nacho. Huyu nyoka hana upanga? Akamwambia, ana upanga, tena mzuri, tena mwema, tena upanga huu ni wa radi. Akamwambia nipe, mama. Akaenda hatta changoni, akiwangua, akija akimpa. Akamwambia, ndiwo huu mama? Akamwambia, ndio huu, mwanangu. Akamwambia, tena upesi, anakuja tena wakati huu, wewe umekuja kujiua wewe, uje uniue na mimi. Akamwambia, kwa nini, mama? Akamwambia, si nnakwambia, huta'mweza. Akamwambia, Kama kufa, tumekwisha kufa, tumesalia kuoza, nawe mama piga moyo konde, nami nijaribu leo, kama hawa wakiwa kindakindaki wafaume wa nyuki, hawaku'mweza nyoka huyu, bassi mimi leo nita'mweza. Akamwambia, Ah! mwanangu.

Marra asikia tufani inavuma. Yule mzee akamwambia, wamsikia mwanamume anakuja? Akamwambia, nami nilio ndani mwanamume, mafahali mawili hayakai zizi moja, atakaa yeye nyumba hii, ao nitakaa mimi. Yule kizee akacheka sana kwa maneno anaotoa yule paa. Yule mzee akaona nafsi yake amekufa, kwani yule kizee, aliwaona watu wanao nguvu marra elfu kuliko huyu paa, nao hawaku'mweza nyoka huyu, aliwashinda. Akamwambia, mama, ache haya, matunda si mazu, mazu ni mwekundu. Bassi saburi, mama.

Marra mbeja wa kani akiwasili nyumbani alikowasili,