Page:Swahili tales.djvu/110

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
90
SULTANI DARAI.

Akapiga mwango konde, akapiga hodi! Akapiga tena, hodi! asipate mtu ndani wa kumjibu. Ah! nyumba hii haina mtu. Mbona mwango haukufungwa kwa 'nje? Labuda wenyewe wamelala, ao labuda wenyewe wako mbali, hawanisikii. Lakini sasa nitapiga hodi sana, wakiwa mbali wanisikie, na kama wamelala waamke.

Akapiga ho-o-o-di! ho-o-o-o-di! Akaitika huko ndani mzee, hodi! Akamwuliza, nani wewe unayopiga hodi? Akamwambia, mimi, bibi mkubwa, mjukuu wako. Akamwambia, kama ni mjukuu wangu, baba, rudi kuko ulikotoka, usije ukafa hapa, ukanijongea na mimi kufa.

Akamwambia, bibi, fungua, nna maneno yangu matatu nataka kukwambia. Akamwambia, mjukuu wangu, sikatai kufungua, nachelea kuponza roho yako, yaponza na yangu. Akamwambia, bibi roho yangu haitakwenda, wala yako haitakwenda, wallakini, bibi mkubwa, tafáthali fungua, nikwambie maneno yangu matatu.

Akafungua mwango yule kizee. Akamwambia, nashika moo, bibi. Akamwambia, marahaba, mjukuu wangu, akamwambia, Je! habari utokako, mjukuu wangu. Akamwambia, bibi mkubwa, nitokako kwema na hapa nijapo pema. Akamwambia, Ah! mwanangu, hapa ndio si pema kabisa, kama wewe watafuta njia ya kufa, wala kama hujaona kufa, bassi leo ndio siku ya kuona kufa, ndio siku ya kujua kufa.

Akamwambia, bibi mkubwa, nzi kufia tuini, si hasara. Akamwambia, yatakapokuwa hayo, mwanangu, mimi nakuonea hasara, kwani wamekufa watu wengi, wana na