Page:Swahili tales.djvu/106

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
86
SULTANI DARAI.

Wakaenda hatta wakakutana, Sultani Darai na mkwewe, wapana mikono, killa mtu akambusu mwenziwe sana, wakafuatana hatta nyumbani.

Walipokwenda hatta nyumbani, akawaambia yule kijana, mtengeni mbali chumba, asichomwona mtu. Kwani mchumbawe amekuja. Sultani pale akaamru chakula, wakaja wakala, wakazumgumza sana, hatta walipokoma wakati wa usiku, akatiwa ndani Sultani Darai, yeye na paa wake, na waaskari watatu kumngojea mwangoni hatta siku ukacha.

Walipokucha usiku paa akaenda, akamwambia Sultani, akamwambia, bwana kazi hii mtu ajiayo ndio atendayo, bassi bwana, twataka utuoze mke wetu, kwani Sultani Darai roho yake na inamkumutika. Akamwambia, tayari mke, kamwiteni mwalimu waje. Akaenda akaita mwalimu akaja. Haya twataka umwoze bwana huyu. Ee wala, tayari. Akitwaa akimwoza. Sultani akaamru kupiga mizinga, ikapigwa mizinga sana. Sultani akaamru kupiga ngoma, killa taifa ipige ngoma yake. Bassi Sultani Darai akaingia nyumbani.

Hatta muda siku ya pili, paa akamwambia bwana wake, mimi ninatoka nasafiri, muda wa siku saba nitarudi, na nisiporudi muda wa siku saba usitoke ndani illa nije. Akamwambia, vema, inshallah. Akamwambia, kua heri sana bwana.

Akaenda akamwaga yule Sultani mwenyi inchi, akamwambia, Bwana. Akamwambia, lebeka, paa. Akamwambia, Sultani Darai amenituma kwenda mjini kwake, kwenda kutengeneza nyumba. Ameniambia, muda wa