Page:Swahili tales.djvu/104

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
84
SULTANI DARAI.

mke, nguo, mgomba na kulimiwa, ndiwo wapo mnono. Akamwambia, bwana wangu, wewe kuko uliko mbali, walipopanda frasi huyo ulivyovaa na kisua hicho, mtu hakujui kama walikuwa jana ukipekua, licha ya huku ugenini twendako tutakaporegea katika inchi yetu tulipotoka, hutaambiwa ndiye maskini aliopekua jaani, watu hatasadiki gissi ulivyokuwa mzuri, gissi ulivyotakata uso. Akamwambia, akali ya neno, na akali ya jawabu, hatta meno yako leo yalivyokuwa meupe, mtu haneni ila mwezi arobatashara ndio mwezi mwenyi wanga. Akamwambia, hiiyote ni takarimu yako walio nikerimu.

Bassi wakaenda zao. Wakaenda—a—a, hatta alipotupa macho yule paa, akaiona ile nyumba ya Sultani. Akamwambia, Bwana wayona nyumba ile? Akamwambia, nimeyona. Akamwambia, bassi ndio nyumba tunaoikwenda, bassi wewe tena huku si maskini, nawe jina lako walijua? Akamwambia, nalijua. Jina lako nani? Akamwambia, nimekwitwa Hamdani. Akamwambia, sili jina lako hilo. Je! baba, jina langu nani? Akamwambia, jina lako Sultani Darai. Akamwambia, vema.

Marra wakawaona asikari wanakuja mbio, na waasikari wangine wakaenda mbio, kwenda kumwambia Sultani. Wakawasili pale waaskari arobatashara, hatta wakienda kidogo, wamwona Sultani, na mawaziri, na maamiri, na makathi, na matajiri yalionao katika mji wanakuja.

Paa akamwambia, Shuka juu ya frasi, bwana, mkwewe anakuja kukulaki, na mkwewe ni yule alio katinakati, yule mwenyi kuvaa joho ya samawi. Akamwambia, vema. Akashuka juu ya frasi, wakaitwa waaskari, wakapokea frasi.