Page:Swahili tales.djvu/100

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
80
SULTANI DARAI.

yule kujua kunena na kuweza kusarifu maneno kwa uzuri. Hatta akachukua frasi yule. Akaamini roho yake yule paa. Frasi ni mkuu kuliko paa, frasi na yule paa, akiinama yule frasi akimtazama paa, huona kama sisi tunavyoona chungu chini, naye frasi ndivyo amwonavyo paa chini yake. Lakini hatutambui busara ya paa yule.

Sultani akanena, Hee! paa yule ametoka katika mkono wa mngwana, katika miango ya Sultani, ametoka katika macho ya watu wenyi nguvu, ndio maana ya paa yule. Akawa mtu bora yeye kwa Sultani huyu.

Bassi akaenda yule paa hatta akafika kwa bwana wake pale alipo, alipomwambia, hapa usiondoke, naye akamkuta palepale, hakuondoka.

Yule bwana aliposikia shindo alipotupa macho nyuma, aona paa na frasi, akacheka sana, hatta paa akifika, akamwambia bwana wake, Hodi! hódi! Akamwambia, Hodi! bwana wangu. Akamwambia, karibu mfathili wangu, karibu msemaji wangu, karibu takarima wangu. Akamwambia, Nimekaa bwana wangu, nimekaa seyedi yangu. Akamwambia, nimekuletea vyakula hivi vitamu. Akamwambia, nivipendavyo vyakula hivi, kwani vyakula vikiwa vitamu vitupu vyakula huwa sumu.

Akamwambia, uondoke bwana, uoge. Akaingia katika mto bwana wake. Akamwambia hapa mtoni maji haba, ingia pale ziwani. Akamwambia, pale ziwani mbona unaogopa, pana maji ungi ungi tele, na pahali panapokuwa na maji ungi tele, panapo ziwa, hapakosi nyama walio adui.

Akamwambia, nyama gani, bwana? Akamwambia, kwanza, katika maziwa hamkosi chatu, na wa pili, ha-