Mungu ibariki Afrika

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search

Mungu Ibariki Afrika ni jina la wimbo wa taifa wa Tanzania. Asili yake ni wimbo wa Nkosi Sikelel' iAfrika wa Afrika Kusini. Enoch Sontonga ndiye mtunzi wa Nkosi Sikelel'i Afrika mwaka 1897. Sehemu ya wimbo huu inatumika pia katika nyimbo za taifa za Afrika Kusini na Zambia. Na huko nyuma ulitumiwa kama wimbo wa taifa wa Zimbabwe.

Mungu ibariki Afrika

Mungu ibariki Afrika
Wabariki viongozi wake
Hekima, Umoja na Amani
Hizi ni ngao zetu
Afrika na watu wake

KIITIKIO:

Ibariki Afrika
Ibariki Afrika
Tubariki watoto wa Afrika
Mungu ibariki Tanzania
Dumisha Uhuru na Umoja
Wake kwa Waume na Watoto
Mungu ibariki Tanzania na watu wake

KIITIKIO:

Ibariki Tanzania
Ibariki Tanzania
Tubariki watoto wa Tanzania

Viungo vya Nje[edit]

Wikipedia logo
Wikipedia logo
Look up Mungu ibariki Afrika in Wikipedia, the free encyclopedia.