Majina ya mji wa Mtume wa Madina

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search

Majina ya mji wa Mtume wa Madina 1. Madina: Amesema Mwenyezi Mungu Aliyetukuka{Wanasema: lau tutarudi Madina watawatoa walio watukufu zaidi wale walio wanyonge zaidi}[63: 8]. 2. Twaba: Amepokewa Jabir bin Samurah t akisema:« Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu(saw) akisema: (Hakika Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Ameipa Madina jina la Twaba)[Imepokewa na Muslim.]. 3. Twayiba: Amepokewa Zaid bin Tahabit t akisema kumpokea Mtume(saw):(Hiyo ni Twayiba, inaondoa dhambi kama ambapo moto unaondoa uchafu wa fedha)[Imepokewaq na Bukhari na Muslim.]. Fadhila za Madina ya Mtume 1. Sa›d bin Abii Waqqaasw t amepokewa akisema kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:(Madina ni bora kwao lau walikuwa wanajua. Haiachi mtu yoyote kwa kutoipenda isipokuwa Mwenyezi Mungu humweka mtu bora kuliko yeye awe ni badala yake. Na yoyote atakayevumilia shida zake [ La’waa’: Shida na dhiki za maisha.] na usumbufu wake, nitakuwa ni muombezi wake au shahidi wake Siku ya Kiyama)[Imepokewa na Muslim.].2. Abu Huraira t amepokewa akisema kwamba Mtume (saw) amesema:(Nimeamrishwa kwenye kitongoji [ Nimeamrishwa kwa kitongoji: nimeamrishwa nigurie hapo, niteremkie hapo na niishi hapo.] kinachokula vitongoji [ Kinachokula vitongoji: watu wake wata washinda watu wa miji mingine na kitakuwa ni kituo cha majeshi ya Kiislamu.], wanakiita Yathrib [ Wanakiita Yathrib: Watu wake walikiita Yathrib wakati wa jahilia, na sasa kinafaa kiitwe Madina.], nayo ni Madina, inawaondoa watu [ Kinawaondoa watu: Kinawatoa wabaya miongoni mwao.], kama vile kiriba [ Kiriba: ni kile kinachovuviwa na mfuzi wa chuma ndani ya moto.] kinvyoondoa uchafu wa chuma [ Uchafu wa chuma: uchafu wake na takataka zake.])[Imepokewa na Bukhaeri na Muslim.]. Miongoni mwa mambo yanayo husu Mji wa Madina 1. Ni mji mtakatifu wa amani kuanzia eneo la ‘Ayr mpaka Thaur. nayo ni majabali mawili. miti yake haikatwi na wanyama wake hawawindwi.Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:(Madina ni takatifu, kuanzia ‘Ayr mpaka Thaur. Basi yoyote mwenye kuzusha uzushi humo au akampa himaya mzushi, itamshukia yeye laana ya Mwenyezi Mungu, Malaika na watu wote)[Imepokewa na Bukhaeri na Muslim.].Na Mtume (saw) Aliujalia mji wa Madina kuwa ni haram kama alivyo ujalia nabii Ibrahim Mji wa Makka, Amepokea Abdullah bin Zeyd kutoka kwa Mtume (saw)(Hakika ibrahim u Alijalia Makka kuwa ni haram na akauwombea, na mimi nimeujalia mji wa madina kuwa ni haram kama alivyo ufanya Ibrahim Makka, na nimeombea katika mudi wake na pishi yake Mfano alivyo ombea nabii Ibrahim mji wa Makka)[Imepokewa na Bukhaeri.]Tafauti ilioko baina haramu ya Makka na haramu ya Madini, nikuwa haram ya Makka imekuja nasi na kwa ijmai ya wanavyooni ama haram ya madina kuna khilafu baina ya wanachuoni lakini kauli sahahi ni kuwa ni haramJabali la ThaurJabali la ‹Ayr2. Kuswali humo thawabu zake zinaongezwa mara nyingi zaidiAmesema Mtume (saw):(Swala moja kwenye msikiti wangu huu ni bora kuliko Swala elfu moja kwenye msikiti mwingine usiokuwa huo, isipokuwa Msikiti wa Haram)[Imepokewa na Bukhaeri.].3. Ndani yake kuna bustani miongoni(saw)mwa mabustani ya Pepo, na imesunniwa kuswali hapo:Abu Huraira t alimpokea Nabii akisema:(Baina ya nyumba yangu na mimbari yangu ni bustani miongoni mwa mabustani ya Peponi, na mimbari yangu iko juu ya Birika (hawdh) yangu)[Imepokewa na Bukhaeri na Muslim.].Raudha tukufu4. Masiih Dajali atakaekuja zama za mwisho hataingia humo, na janga la maradhi mabaya ya kuenea na kuua: [ Twaa›uun: maradhi mabaya.]Anas bin Malik amepokewa akisema kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema:(Dajali atakuja Madina awakute Malaika wanaulinda. Basi ugonjwa hatari wa kuambukiuza hautaingia humo wala Dajali hataingia, Mwenyezi Mungu Akitaka)[Imepokewa na Tirmidhi.].5. Mtume(saw) aliuombea mji wa Madina baraka:Anas t alisema kwamba Nabii(saw) alisema:(Ewe Mola! Ijaalie Madina baraka mara mbili zaidi ya ulivyoijaalia Makka)[Imepokewa na Bukhaeri na Muslim.].6. kuwinda Makka mtu hupata madhambi na atalipa na kuwinda Madina mtu hupata madhambi lakini halazimiki na kitu chochote na madhambi ya kuwinda makka ni makubwa zaidi kuliko kuwinda Madina[Tazama Almumti’ juzuu ya 7-ukurasa 257]

viungo vya nje[edit]