Itikafu(kukaa ndani ya msikiti)

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search

Mambo yenye kuharibu Itikafu 1. Kutoka msikitini bila ya dharura yoyote kwa kukusudia – hata kama kipindi ulichotoka ni kichache kiasi gani -; Kama ilivyothibi kutoka kwa A’isha t akisema: (Na alikuwa (Mtume) haingii nyumbani isipokuwa kwa haja ya kibinadamu) [Imepokewa na Muslim.].

Na kwasababu kule kutoka kuna acha kipindi fulani kukosekana kwa mwenye kufanya Itikafu ndani ya msikiti, na huku kuwa ndani ya msikiti ni nguzo ya Itikafu.

2. Kufanya tendo la ndoa – hata kama kufanya huko kutakuwa ni usiku. Kwa kauli ya Mwenyezi Mungu U: {Wala msichanganyike nao, na hali mnakaa Itikafu misikitini} (Al-Baqarah – Aya 187).

Na hukumu hii ya tendo la ndoa pia inasimamia: Kuondosha matamanio bila ya kuingiliana kama kujitoa manii kwa kutumia mkono, na kumshikashika mkeo sehemu zisizo za siri.

3. Kuwa na niya ya kuivunja Itikafu. Anaponuia Muislamu kufanya Itikafu siku maalumu, kisha akavunja kuifanya hiyo Itikafu yuwafaa ailipe, kama ilivyothibiti kutoka kwa A’isha – Mungu awe naye radhi asema: (Alikuwa Mtume (saw) anapotaka kufanya Itikafu akiswali alfajiri kisha ndio aingie mahali pake pa itikafu [ Mahali pake pa Itikafu: Yaani sehemu anayokaa kufanyia Itikafu.]. Na hakika aliamrisha kufungwa khibai (hema) lake na likafungwa – Hali ya kutaka kufanya Itikafu kumi la mwisho la mwezi wa Ramadhani -; Zainab naye aliamrisha kufungwa khibai lake na likafungwa. Na aliamrisha mwengine katika wake za Mtume (saw) kufungwa khibai lake na likafungwa. Mtume alipomaliza kuswali alfajiri akatizama, akaona makhibai (mahema). Akasema: Ni wema munataka? Akachukua khibai lake akalinyanyua [ Kulinyanyua: Yaani kulikunjakunja lile khibai.]. Na akaacha Itikafu katika Ramadhani mpaka kumi la kwanza la mwezi wa Shawwal” [Imepokewa na Bukhari na Muslim]. Na katika upokezi mwengine: (kumi la mwisho la mwezi wa Shawwal).

4. Mwenye kufanya Itikafu hatembelei mgonjwa wala hashindikizi jeneza. Na yuwabaki kufanya ibada mahali pake pa Itikafu.

viungo vya nje[edit]

[1]

itikafu